Ni Kikundi cha Kijamii cha Kimaendeleo ya kijamii na Kiuchumi (Community Based Organisation) na kinajihusisha na kusaidiana kwenye shida na raha, Kikundi hiki kipo kwa kutimiza au kutekeleza yafuatayo:-
Aidha kikundi hiki ni cha hiari chenye lengo la kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa ustawi wa wanachama wake. Kikundi hiki kimeanzishwa rasmi tarehe 01 AGOSTI 2021. UMOJA WA WANYAMBO KARAGWE NA KYERWA (UWKK) ni kikundi kilichoanzishwa na vijana wa Kinyambo wa KARAGWE NA KYERWA wanaoishi mkoa wa Dar es Salaam. Tunakaribisha WANYAMBO WA KARAGWE NA KYERWA waliopo popote nchini na hata nje ya nchi (Tanzania) kujiunga nasi.
Kushirikiana kufanya miradi mbalimbali ya Kiuchumi na Kijamii kwa maendeleo ya kikundi na ustawi wa wanachama.